Tuesday, 29 March 2016

KLIMO UTI WAMGONGO WA TAIFA



KILIMO ni uti wa mgongo wa taifa. Kauli mbiu hiyo imechangia kuweka mikakati mingi ya kuendeleza kilimo sambamba na kauli mbiu tofauti kama, ‘Siasa ni Kilimo’, ‘Kilimo Kwanza’ na ‘kilimo cha kufa na kupona’. Kwa misingi hiyo, Watanzania hawawezi kukwepa suala la kilimo kwa vile bado ni njia kuu ya kujenga uchumi wa taifa na kuharakisha maendeleo ya mmoja mmoja. Kilimo cha mtu mmoja mmoja vijijini mpaka sasa hakijaleta mafanikio makubwa kutokana na kutumia zana duni ingawa wakulima wachache wamekiri kupata mafanikio. Wakulima wengi wadogo hawajapata mafanikio kwa kuwa Serikali haijaweka mikakati madhubuti ya kulima kisasa na kuwatafutia masoko.

No comments:

Post a Comment